Agano la Kale

Agano Jipya

Yeremia 10:4-11 Biblia Habari Njema (BHN)

4. Kisha watu hukipamba kwa fedha na dhahabuwakakipigilia misumari kwa nyundoili kisije kikaanguka.

5. Vinyago vyao ni kama vinyago vya kutishia ndegekatika shamba la matango,havina uwezo wa kuongea;ni lazima vibebwemaana haviwezi kutembea.Msiviogope vinyago hivyo,maana haviwezi kudhuru,wala haviwezi kutenda lolote jema.”

6. Ee Mwenyezi-Mungu, hakuna aliye kama wewe;wewe ni mkuu na nguvu yako yajulikana.

7. Nani asiyekuogopa wewe, ee mfalme wa mataifa?Wewe wastahili kuheshimiwa.Miongoni mwa wenye hekima wote wa mataifa,na katika falme zao zote,hakuna hata mmoja aliye kama wewe.

8. Wote ni wajinga na wapumbavumafunzo ya vinyago ni upuuzi mtupu!

9. Vinyago hivyo hupambwa kwa fedha kutoka Tarshishi,na dhahabu kutoka Ofiri;kazi ya mafundi stadi na wafua dhahabu.Zimevishwa nguo za samawati na zambarau,zilizofumwa na wafumaji stadi.

10. Lakini Mwenyezi-Mungu ni Mungu wa kweli;Mungu aliye hai, mfalme wa milele.Akikasirika, dunia hutetemeka,mataifa hayawezi kustahimili hasira yake.

11. Basi, utawaambia hivi: “Miungu ambayo haikuumba mbingu na dunia, itaangamia. Itatoweka kabisa duniani na chini ya mbingu.”

Kusoma sura kamili Yeremia 10