Agano la Kale

Agano Jipya

Wimbo Ulio Bora 7:5-12 Biblia Habari Njema (BHN)

5. Kichwa chako juu yako ni kama mlima Karmeli,nywele zako za ukoka zangaa kama zambarau;uzuri wako waweza kumteka hata mfalme.

6. Tazama ulivyo mzuri na wa kuvutia!Ewe mpenzi, mwali upendezaye!

7. Umbo lako lapendeza kama mtende,matiti yako ni kama shada za tende.

8. Nilisema nitaupanda mtende na kuzichuma shada za tende.Kwangu matiti yako ni kama shada za zabibu,harufu nzuri ya pumzi yako ni kama matofaa;

9. na kinywa chako ni kama divai tamu.Basi divai na itiririke hadi kwa mpenzi wangu,ipite juu ya midomo yake na meno yake!

10. Mimi ni wake mpenzi wangu,naye anionea sana shauku.

11. Njoo ewe mpenzi wangu, twende mashambani,twende zetu tukalale huko vijijini.

12. Tutaamka mapema, twende kwenye mashamba ya mizabibu,tukaone kama imeanza kuchipua,na kama maua ya zabibu yamekwisha kuchanua,pia kama mikomamanga imeanza kutoa maua.Huko ndiko nitakapokupatia pendo langu.

Kusoma sura kamili Wimbo Ulio Bora 7