Agano la Kale

Agano Jipya

Wimbo Ulio Bora 7:3-9 Biblia Habari Njema (BHN)

3. Matiti yako ni kama paa mapacha,ni kama swala wawili.

4. Shingo yako ni kama mnara wa pembe za ndovu;macho yako ni kama vidimbwi mjini Heshboni,karibu na mlango wa Beth-rabi.Pua yako ni kama mnara wa Lebanoni,ambao unauelekea mji wa Damasko.

5. Kichwa chako juu yako ni kama mlima Karmeli,nywele zako za ukoka zangaa kama zambarau;uzuri wako waweza kumteka hata mfalme.

6. Tazama ulivyo mzuri na wa kuvutia!Ewe mpenzi, mwali upendezaye!

7. Umbo lako lapendeza kama mtende,matiti yako ni kama shada za tende.

8. Nilisema nitaupanda mtende na kuzichuma shada za tende.Kwangu matiti yako ni kama shada za zabibu,harufu nzuri ya pumzi yako ni kama matofaa;

9. na kinywa chako ni kama divai tamu.Basi divai na itiririke hadi kwa mpenzi wangu,ipite juu ya midomo yake na meno yake!

Kusoma sura kamili Wimbo Ulio Bora 7