Agano la Kale

Agano Jipya

Wimbo Ulio Bora 7:10-13 Biblia Habari Njema (BHN)

10. Mimi ni wake mpenzi wangu,naye anionea sana shauku.

11. Njoo ewe mpenzi wangu, twende mashambani,twende zetu tukalale huko vijijini.

12. Tutaamka mapema, twende kwenye mashamba ya mizabibu,tukaone kama imeanza kuchipua,na kama maua ya zabibu yamekwisha kuchanua,pia kama mikomamanga imeanza kutoa maua.Huko ndiko nitakapokupatia pendo langu.

13. Harufu nzuri ya tunguja imejaa hewanikaribu na milango yetu kuna kila aina ya matunda bora,yote mapya na ya siku za nyuma,ambayo nimekuwekea wewe mpenzi wangu.

Kusoma sura kamili Wimbo Ulio Bora 7