Agano la Kale

Agano Jipya

Wimbo Ulio Bora 7:1-4 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Nyayo zako katika viatu zapendeza sana!Ewe mwanamwali wa kifalme.Mapaja yako ya mviringo ni kama johari,kazi ya msanii hodari.

2. Kitovu chako ni kama bakulilisilokosa divai iliyokolezwa.Tumbo lako ni kama lundo la nganolililozungushiwa yungiyungi kandokando.

3. Matiti yako ni kama paa mapacha,ni kama swala wawili.

4. Shingo yako ni kama mnara wa pembe za ndovu;macho yako ni kama vidimbwi mjini Heshboni,karibu na mlango wa Beth-rabi.Pua yako ni kama mnara wa Lebanoni,ambao unauelekea mji wa Damasko.

Kusoma sura kamili Wimbo Ulio Bora 7