Agano la Kale

Agano Jipya

Wimbo Ulio Bora 6:7-13 Biblia Habari Njema (BHN)

7. Mashavu yako ni kama nusu mbili za komamanga,nyuma ya shela lako.

8. Wapo malkia sitini, masuria themanini,na wasichana wasiohesabika!

9. Hua wangu, mzuri wangu, ni mmoja tu,na ni kipenzi cha mama yake;yeye ni wa pekee kwa mama yake.Wasichana humtazama na kumwita heri,nao malkia na masuria huziimba sifa zake.

10. Nani huyu atazamaye kama pambazuko?Mzuri kama mwezi, mwangavu kama jua,na anatisha kama jeshi lenye bendera.

11. Nimeingia katika bustani ya milozikutazama machipuko ya bondeni,kuona kama mizabibu imechanua,na mikomamanga imechanua maua.

12. Bila kutazamia, mpenzi wangu,akanitia katika gari la mkuu.

13. Rudi, rudi ewe msichana wa Mshulami.Rudi, rudi tupate kukutazama.Mbona mwataka kunitazama miye Mshulamikana kwamba mnatazama ngomakati ya majeshi mawili?

Kusoma sura kamili Wimbo Ulio Bora 6