Agano la Kale

Agano Jipya

Wimbo Ulio Bora 6:1-5 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Ewe mwanamke uliye mzuri sana;amekwenda wapi huyo mpenzi wako?Ameelekea wapi mpenzi wakoili tupate kushirikiana nawe katika kumtafuta?

2. Mpenzi wangu amekwenda bustanini mwake,mahali ambapo rihani hustawi.Yeye analisha kondoo wakena kukusanya yungiyungi.

3. Mimi ni wake mpenzi wangu, naye ni wangu;yeye huwalisha kondoo wake penye yungiyungi.

4. Mpenzi wangu, wewe u mzuri kama Tirza,wapendeza kama Yerusalemu,unatisha kama jeshi lenye bendera.

5. Hebu tazama kando tafadhali;ukinitazama nahangaika.Nywele zako ni kama kundi la mbuzi,wateremkao chini ya milima ya Gileadi.

Kusoma sura kamili Wimbo Ulio Bora 6