Agano la Kale

Agano Jipya

Wimbo Ulio Bora 5:1-7 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Naingia bustanini mwangu,dada yangu, bi arusi.Nakusanya manemane na viungo,nala sega langu la asali,nanywa divai yangu na maziwa yangu.Kuleni enyi marafiki, kunyweni;kunyweni sana wapendwa wangu.

2. Nililala, lakini moyo wangu haukulala.Sauti ya mpenzi wangu anabisha hodi.“Nifungulie, dada yangu mpenzi wangu, bibiarusi wangu,hua wangu, usiye na kasoro.Kichwa changu kimelowa umandena nywele zangu manyunyu ya usiku.”

3. Nimekwisha yavua mavazi yangu,nitayavaaje tena?Nimekwisha nawa miguu yangu,niichafueje tena?

4. Hapo mpenzi wangu akaugusa mlango,moyo wangu ukajaa furaha.

5. Niliinuka kumfungulia mpenzi wangu.Mikono yangu imejaa manemane,na vidole vyangu vyadondosha manemane,nilipolishika komeo kufungua mlango.

6. Nilimfungulia mlango mpenzi wangu,lakini kumbe, alikuwa amekwisha toweka.Moyo wangu ulifurahi alipokuwa akizungumza!Nilimtafuta, lakini sikumpata;nilimwita, lakini hakuniitikia.

7. Walinzi wa mji waliniona,walipokuwa wanazunguka mjini;wakanipiga na kunijeruhi;nao walinzi wa lango wakaninyanganya shela langu.

Kusoma sura kamili Wimbo Ulio Bora 5