Agano la Kale

Agano Jipya

Wimbo Ulio Bora 4:12-16 Biblia Habari Njema (BHN)

12. Dada yangu, naam, bi arusi,ni bustani iliyofichika,bustani iliyosetiriwa;chemchemi iliyotiwa mhuri.

13. Machipukizi yako ni bustani ya mikomamangapamoja na matunda bora kuliko yote,hina na nardo.

14. Nardo na zafarani, mchai na mdalasinimanemane na udi,na mimea mingineyo yenye harufu nzuri.

15. U chemchemi ya bustani,kisima cha maji yaliyo hai,vijito vitiririkavyo kutoka Lebanoni.

16. Vuma, ewe upepo wa kaskazi,njoo, ewe upepo wa kusi;vumeni juu ya bustani yangu,mlijaze anga kwa manukato yake.Mpenzi wangu na aje bustanini mwake,ale matunda yake bora kuliko yote.

Kusoma sura kamili Wimbo Ulio Bora 4