Agano la Kale

Agano Jipya

Wimbo Ulio Bora 3:7-11 Biblia Habari Njema (BHN)

7. Tazama! Ni machela ya Solomoni;amebebwa juu ya kiti chake cha enzi;amezungukwa na walinzi sitini,mashujaa bora wa Israeli.

8. Kila mmoja wao ameshika upanga,kila mmoja wao ni hodari wa vita.Kila mmoja ana upanga wake mkononi,tayari kumkabili adui usiku.

9. Mfalme Solomoni alijitengenezea machela,kwa mbao nzuri kutoka Lebanoni.

10. Nguzo zake zilitengenezwa kwa fedha;mgongo wake kwa dhahabu;mahali pa kukalia pamefunikwa vitambaa vya zambarau,walichoshona kwa upendo wanawake wa Yerusalemu,waliokishonea alama za upendo.

11. Njoni basi enyi wanawake wa Siyoni,mkamwone mfalme Solomoni.Amevalia taji aliyovikwa na mama yake,siku alipofanya harusi yake,naam, siku ambayo moyo wake ulijaa furaha.

Kusoma sura kamili Wimbo Ulio Bora 3