Agano la Kale

Agano Jipya

Wimbo Ulio Bora 2:8-17 Biblia Habari Njema (BHN)

8. Hiyo ni sauti ya mpenzi wangu,yuaja mbio,anaruka milima,vilima anavipita kasi!

9. Mpenzi wangu ni kama paa,ni kama swala mchanga.Amesimama karibu na ukuta wetu,achungulia dirishani,atazama kimiani.

10. Mpenzi wangu aniambia:“Inuka basi, ewe mpenzi wangu, unipendezaye,njoo twende zetu.

11. Tazama, majira ya baridi yamepita,nazo mvua zimekwisha koma;

12. maua yamechanua kila mahali.Wakati wa kuimba umefika;sauti ya hua yasikika mashambani mwetu.

13. Mitini imeanza kuzaa;na mizabibu imechanua;inatoa harufu nzuri.Njoo, basi, ewe mpenzi wangu unipendezaye,njoo twende.

14. Ee hua wangu, uliyejificha miambani.Hebu niuone uso wako,hebu niisikie sauti yako,maana sauti yako yapendeza na uso wako wavutia.

15. “Tukamatieni mbweha,wale mbweha wadogowadogo,wanaoiharibu mizabibu yetu inayochanua.”

16. Mpenzi wangu ni wangu, nami ni wake.Yeye hulisha kondoo wake penye yungiyungi,

17. hadi hapo jua linapochomozana vivuli kutoweka.Rudi kama paa mpenzi wangu,kama swala mdogo juu ya milima ya Betheri.

Kusoma sura kamili Wimbo Ulio Bora 2