Agano la Kale

Agano Jipya

Wimbo Ulio Bora 1:1-4 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Wimbo wa Solomoni ulio bora kuliko nyimbo zote.

2. Heri midomo yako inibusu,maana pendo lako ni bora kuliko divai.

3. Manukato yako yanukia vizuri,na jina lako ni kama marashi yaliyomiminwa.Kwa hiyo wanawake hukupenda!

4. Nichukue, twende zetu haraka,mfalme amenileta katika chumba chake.Tutafurahi na kushangilia kwa sababu yako,tutasifu mapenzi yako kuliko divai.Wanawake wana haki kukupenda!

Kusoma sura kamili Wimbo Ulio Bora 1