Agano la Kale

Agano Jipya

Waamuzi 5:24-30 Biblia Habari Njema (BHN)

24. “Abarikiwe kuliko wanawake woteYaeli, mke wa Heberi, Mkeni.Naam, amebarikiwa kuliko wanawake wotewanaokaa mahemani.

25. Sisera alimwomba maji, naye akampa maziwa;alimletea siagi katika bakuli ya heshima.

26. Kwa mkono mmoja alishika kigingi cha hema,na kwa mkono wake wa kulia nyundo ya fundi;alimponda Sisera kichwa,alivunja na kupasuapasua paji lake.

27. Sisera aliinama, akaanguka;alilala kimya miguuni pake.Hapo alipoinama ndipo alipoanguka, amekufa!

28. “Mama yake Sisera alitazama dirishanialichungulia katika viunzi vyake, akalalamika:‘Kwa nini gari lake limechelewa?Mbona vishindo vya magari yake vimechelewa kusikika?’

29. Jibu akalipata kwa wanawake wenye hekima:Akajituliza tena na tena kwa jibu hilo:

30. ‘Bila shaka wanatafuta na kugawana nyara;msichana mmoja au wawili kwa kila askari,vazi la sufu ya rangi kwa ajili ya Sisera.Vazi la sufu iliyotariziwa,na mikufu miwili ya nakshi kwa ajili ya shingo yangu!’

Kusoma sura kamili Waamuzi 5