Agano la Kale

Agano Jipya

Waamuzi 5:13-23 Biblia Habari Njema (BHN)

13. Mashujaa waliobaki waliteremka,watu wa Mwenyezi-Mungu walikwenda kumpiganiadhidi ya wenye nguvu.

14. Kutoka Efraimu waliteremka bondeni,wakafuata ndugu zao watu wa Benyamini;kutoka Makiri walishuka makamanda,kutoka Zebuluni maofisa wakuu.

15. Wakuu wa Isakari wakafuatana na Debora,watu wa Isakari waaminifu kwa Baraki;wakamfuata mbio mpaka bondeni.Lakini miongoni mwa koo za Reubenikulikuwamo kusitasita kwingi.

16. Kwa nini walibaki mazizini?Ili kusikiliza milio ya kondoo?Miongoni mwa koo za Reubenikulikuwamo kusitasita kwingi.

17. Kabila la Gileadi lilibaki ngambo ya Yordani.Kabila la Dani, kwa nini mlibaki merikebuni?Kabila la Asheri lilitulia huko pwani ya bahari,lilikaa bandarini mwake.

18. Watu wa Zebuluni ni watuwaliohatarisha maisha yao katika kifo.Hata wa Naftali walikikabili kifokwenye miinuko ya mashamba.

19. “Huko Taanaki, kando ya chemchemi za Megido,wafalme walikuja, wakapigana;wafalme wa Kanaani walipigana,lakini hawakupata nyara za fedha.

20. Nyota kutoka mbinguni zilishiriki vita,zilifuata njia zao, zilipigana na Sisera.

21. Mafuriko ya mto Kishoni yaliwachukua mbali,naam, mafuriko makali ya mto Kishoni.Songa mbele kwa nguvu, ee nafsi yangu!

22. “Farasi walipita wakipiga shoti;,walikwenda shoti na kishindo cha kwato zao.

23. Malaika wa Mwenyezi-Mungu asema hivi:‘Uapizeni mji wa Merosi,waapizeni vikali wakazi wake;maana hawakuja kumsaidia Mwenyezi-Munguhawakumsaidia Mwenyezi-Mungu dhidi ya wenye nguvu’.

Kusoma sura kamili Waamuzi 5