Agano la Kale

Agano Jipya

Waamuzi 16:1-4 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Siku moja Samsoni alikwenda mjini Gaza, akakutana na malaya mmoja akalala naye.

2. Watu wa Gaza walipoambiwa kuwa Samsoni yuko huko, walilizingira eneo hilo na kumvizia kwenye lango la mji usiku kucha. Wakakaa kimya huko langoni usiku wote wakifikiri kwamba wanaweza kungojea mpaka mapambazuko wapate kumuua.

3. Lakini Samsoni akabaki mjini mpaka usiku wa manane. Wakati wa usiku wa manane akaamka akashika miimo miwili ya malango, akaingoa pamoja na makomeo yake akaibeba na kwenda nayo mpaka karibu na Hebroni.

4. Baada ya hayo, Samsoni alimpenda mwanamke mmoja aitwaye Delila ambaye aliishi katika bonde la Soreki.

Kusoma sura kamili Waamuzi 16