Agano la Kale

Agano Jipya

Waamuzi 15:15-20 Biblia Habari Njema (BHN)

15. Samsoni akapata utaya mbichi wa punda, akautumia kuwaua watu 1,000.

16. Kisha Samsoni akasema,“Kwa utaya wa punda,nimeua watu elfu moja.Kwa utaya wa punda,nimekusanya marundo ya maiti.”

17. Alipomaliza kusema, akatupa utaya huo. Mahali hapo pakaitwa Ramath-lehi, yaani mlima wa utaya.

18. Kisha Samsoni akashikwa na kiu sana. Basi, akamwomba Mwenyezi-Mungu, akisema, “Ee Mungu, wewe ndiwe uliyeleta ukombozi huu, kwa kunitumia mimi mtumishi wako. Je, sasa utaniacha nife kwa kiu na kutekwa na Wafilisti hawa wasiotahiriwa?”

19. Mungu akafungua mahali palipokuwa na shimo huko Leki, akatiririsha maji. Samsoni akanywa maji hayo na nguvu zake zikamrudia. Chemchemi hiyo ikaitwa En-hakore; nayo iko huko Lehi mpaka leo.

20. Samsoni alikuwa mwamuzi wa Waisraeli kwa miaka ishirini, nyakati za Wafilisti.

Kusoma sura kamili Waamuzi 15