Agano la Kale

Agano Jipya

Nehemia 9:4-15 Biblia Habari Njema (BHN)

4. Kuliwekwa jukwaa la Walawi; hapo walisimama Yeshua, Bani, Kadmieli, Shebania, Buni, Sherebia, Bani na Kenani. Wakamwomba kwa sauti kubwa Mwenyezi-Mungu, Mungu wao.

5. Walawi, yaani: Yeshua, Kadmieli, Bani, Hashabuea, Sherebia, Hodia, Shebania na Pethahia wakawaambia watu;“Simameni na kumsifu Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu.Msifuni milele na milele!Na watu walisifu jina lako tukufu,ambalo hutukuka kuliko baraka na sifa zote.”

6. Ezra akaomba kwa sala ifuatayo:“Wewe peke yako ndiwe Mwenyezi-Mungu;ndiwe uliyefanya mbingu na jeshi lake lote,dunia na vyote vilivyomo,bahari na vyote vilivyomo;nawe ndiwe unayevihifadhi hai,na jeshi lote la mbinguni lakuabudu wewe.

7. Wewe ndiwe Mwenyezi-Mungu,Mungu uliyemchagua Abramu,ukamtoa toka Uri ya Wakaldayona kumpa jina Abrahamu.

8. Ukamwona kuwa yu mwadilifu mbele yako;ukafanya agano naye kuwapa wazawa wake nchi ya Wakanaani,Wahiti, Waamori, Waperizi, Wayebusi na Wagirgashi.Na ahadi yako ukaitimiza;kwani wewe u mwaminifu.

9. “Uliyaona mateso ya babu zetuwalipokuwa nchini Misri,na walipokuomba msaada kwenye Bahari ya Shamuuliwasikia.

10. Ulifanya ishara na maajabu dhidi ya Farao,watumishi wake wotena watu wote wa nchi yake;kwani ulijua kuwawaliwakandamiza babu zetu.Ukajipatia umaarufu uliopo mpaka leo.

11. Uliigawa bahari katikati mbele yao,nao wakapita katikati ya bahari,mahali pakavu.Lakini ukawatupa Wamisri waliowafuatiakama jiwe zito ndani ya maji mengi.

12. Mchana uliwaongoza kwa mnara wa wingu,na usiku uliwaongoza kwa mnara wa motoili kuwamulikia njia ya kuendea.

13. Kule mlimani Sinaiulishuka toka mbinguni na kuzungumza nao.Ukawapa maagizo safi, sheria za kweli,kanuni nzuri na amri.

14. Kwa njia ya Mose, mtumishi wako,ukawajulisha Sabato yako takatifuna ukawaagiza kuzifuata amri,kanuni na sheria ulizowaamrisha.

15. Walipokuwa na njaa,ukawapa chakula kutoka mbinguni.Walipokuwa na kiuukawapa maji kutoka kwenye mwamba.Ukawaagiza kuichukua nchi uliyokuwa umewaahidi.

Kusoma sura kamili Nehemia 9