Agano la Kale

Agano Jipya

Nehemia 9:29-38 Biblia Habari Njema (BHN)

29. Ukawaonya ili wairudie sheria yako.Hata hivyo, kwa kiburi chao,wakaacha kuzitii amri zako.Wakayaasi maagizo yako,ambayo kwayo mtu akiyatii, ataishi.Wakawa wajeuripia wakafanya shingo zao ngumu,na wakakataa kuwa watiifu.

30. Ukawavumilia kwa miaka mingi,na kuwaonya kwa njia ya roho yakokwa kupitia manabii wako;hata hivyo hawakusikiliza.Basi ukawaachaukawatia mikononi mwa mataifa mengine.

31. Hata hivyo,kutokana na huruma zako nyingi,hukuwaacha waangamie kabisa au kuwatupa,kwani wewe u Mungu mwenye neemana huruma.

32. Kwa hiyo, ee Mungu wetu,Mungu Mkuu,mwenye nguvu na wa kutisha,wewe unalishika agano lakona una fadhili nyingi.Mateso yaliyotupata, sisi,wafalme wetu, wakuu wetu,makuhani wetu, manabii wetu,babu zetu na watu wako wotetangu wakati wa wafalme wa Ashuru mpaka leo,usiyaone kuwa ni madogo.

33. Hata hivyo,unayo haki kwa kutuadhibu hivyo;kwani wewe umekuwa mwaminifuambapo sisi tumekuwa watenda maovu.

34. Wafalme wetu, wakuu wetu,makuhani wetu na babu zetuhawajaishika sheria yakowala kujali amri yakona maonyo yako uliyowapa.

35. Hawakukutumikia katika ufalme wao,wala walipoyafurahia mema yako mengi uliyowajalia kwa wingi,katika nchi kubwa na yenye rutuba uliyowapahawakuyaacha matendo yao maovu.

36. Na leo tumekuwa watumwa;tu watumwa katika nchi uliyowapa babu zetuwafurahie matunda na vipawa vyake vyema.

37. Kwa sababu ya dhambi zetu,utajiri wa nchi hiiunawaendea wafalme uliowaleta kututawala.Wanatutawala wapendavyohata na mifugo yetuwanaitendea wapendavyo,tumo katika dhiki kuu.”

38. Kutokana na haya yote yaliyotokea, sisi tunaweka agano imara na wakuu wetu kwa maandishi; Walawi na makuhani wanatia sahihi zao na mhuri wao.

Kusoma sura kamili Nehemia 9