Agano la Kale

Agano Jipya

Nehemia 9:25-36 Biblia Habari Njema (BHN)

25. Miji yenye ngome wakaiteka,wakachukua nchi yenye utajiri,majumba yenye vitu vingi vizuri,visima vilivyochimbwa,mashamba ya mizabibu na mizeitunipamoja na miti yenye matunda kwa wingi.Hivyo wakala,wakashiba na kunenepana kuufurahia wema wako.

26. Lakini hawakuwa waaminifu kwako.Wakakuasi,wakaiacha sheria yakona kuwaua manabii waliowaonyaili wakurudie wewe.Wakakufuru sana.

27. Hivyo, ukawatia katika mikono ya adui zao,nao wakawatesa.Lakini wakiwa katika mateso yao,wakakulilia, nawe ukawasikia kutoka mbinguni.Na kwa huruma zako nyingi,ukawapelekea viongozi wa kuwaokoa;nao wakawakomboa toka mikononi mwao.

28. Lakini amani ilipopatikanawakatenda dhambi tena mbele yako,nawe ukawaacha watiwe katikamikono ya adui zao wawatawale.Hata hivyo, walipotubu na kukuliliaukawasikiliza kutoka mbinguni.Na kwa kulingana na huruma zako nyingi,ukawaokoa mara nyingi.

29. Ukawaonya ili wairudie sheria yako.Hata hivyo, kwa kiburi chao,wakaacha kuzitii amri zako.Wakayaasi maagizo yako,ambayo kwayo mtu akiyatii, ataishi.Wakawa wajeuripia wakafanya shingo zao ngumu,na wakakataa kuwa watiifu.

30. Ukawavumilia kwa miaka mingi,na kuwaonya kwa njia ya roho yakokwa kupitia manabii wako;hata hivyo hawakusikiliza.Basi ukawaachaukawatia mikononi mwa mataifa mengine.

31. Hata hivyo,kutokana na huruma zako nyingi,hukuwaacha waangamie kabisa au kuwatupa,kwani wewe u Mungu mwenye neemana huruma.

32. Kwa hiyo, ee Mungu wetu,Mungu Mkuu,mwenye nguvu na wa kutisha,wewe unalishika agano lakona una fadhili nyingi.Mateso yaliyotupata, sisi,wafalme wetu, wakuu wetu,makuhani wetu, manabii wetu,babu zetu na watu wako wotetangu wakati wa wafalme wa Ashuru mpaka leo,usiyaone kuwa ni madogo.

33. Hata hivyo,unayo haki kwa kutuadhibu hivyo;kwani wewe umekuwa mwaminifuambapo sisi tumekuwa watenda maovu.

34. Wafalme wetu, wakuu wetu,makuhani wetu na babu zetuhawajaishika sheria yakowala kujali amri yakona maonyo yako uliyowapa.

35. Hawakukutumikia katika ufalme wao,wala walipoyafurahia mema yako mengi uliyowajalia kwa wingi,katika nchi kubwa na yenye rutuba uliyowapahawakuyaacha matendo yao maovu.

36. Na leo tumekuwa watumwa;tu watumwa katika nchi uliyowapa babu zetuwafurahie matunda na vipawa vyake vyema.

Kusoma sura kamili Nehemia 9