Agano la Kale

Agano Jipya

Nehemia 9:1-12 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Siku ya ishirini na nne ya mwezi huo wa saba, watu wa Israeli walikusanyika, wakifunga na kuvaa mavazi ya magunia na kujipaka udongo kichwani kuonesha majuto yao.

2. Wakati huo, walikuwa wamejitenga mbali na watu wa mataifa mengine, wakasimama na kuungama dhambi zao na maovu ya babu zao.

3. Kwa muda wa kama masaa matatu, walisimama huku sheria ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wao, inasomwa. Na kwa masaa matatu yaliyofuata, walikuwa wakitubu na kumwabudu Mwenyezi-Mungu, Mungu wao.

4. Kuliwekwa jukwaa la Walawi; hapo walisimama Yeshua, Bani, Kadmieli, Shebania, Buni, Sherebia, Bani na Kenani. Wakamwomba kwa sauti kubwa Mwenyezi-Mungu, Mungu wao.

5. Walawi, yaani: Yeshua, Kadmieli, Bani, Hashabuea, Sherebia, Hodia, Shebania na Pethahia wakawaambia watu;“Simameni na kumsifu Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu.Msifuni milele na milele!Na watu walisifu jina lako tukufu,ambalo hutukuka kuliko baraka na sifa zote.”

6. Ezra akaomba kwa sala ifuatayo:“Wewe peke yako ndiwe Mwenyezi-Mungu;ndiwe uliyefanya mbingu na jeshi lake lote,dunia na vyote vilivyomo,bahari na vyote vilivyomo;nawe ndiwe unayevihifadhi hai,na jeshi lote la mbinguni lakuabudu wewe.

7. Wewe ndiwe Mwenyezi-Mungu,Mungu uliyemchagua Abramu,ukamtoa toka Uri ya Wakaldayona kumpa jina Abrahamu.

8. Ukamwona kuwa yu mwadilifu mbele yako;ukafanya agano naye kuwapa wazawa wake nchi ya Wakanaani,Wahiti, Waamori, Waperizi, Wayebusi na Wagirgashi.Na ahadi yako ukaitimiza;kwani wewe u mwaminifu.

9. “Uliyaona mateso ya babu zetuwalipokuwa nchini Misri,na walipokuomba msaada kwenye Bahari ya Shamuuliwasikia.

10. Ulifanya ishara na maajabu dhidi ya Farao,watumishi wake wotena watu wote wa nchi yake;kwani ulijua kuwawaliwakandamiza babu zetu.Ukajipatia umaarufu uliopo mpaka leo.

11. Uliigawa bahari katikati mbele yao,nao wakapita katikati ya bahari,mahali pakavu.Lakini ukawatupa Wamisri waliowafuatiakama jiwe zito ndani ya maji mengi.

12. Mchana uliwaongoza kwa mnara wa wingu,na usiku uliwaongoza kwa mnara wa motoili kuwamulikia njia ya kuendea.

Kusoma sura kamili Nehemia 9