30. wa miji ya Rama na Geba: 621;
31. wa mji wa Mikmashi: 122;
32. wa miji ya Betheli na Ai: 123;
33. wa mji mwingine wa Nebo: 52;
34. wa mji mwingine wa Elamu: 1,254;
35. wa mji wa Harimu: 320;
36. wa mji wa Yeriko: 345;
37. wa miji ya Lodi, Hadidi na Ono: 721;
38. wa mji wa Senaa: 3,930.
39. Ifuatayo ni idadi ya makuhani waliorudi kutoka uhamishoni: Makuhani wa ukoo wa Yedaya, waliokuwa wazawa wa Yeshua: 973;
40. wa ukoo wa Imeri: 1,052;
41. wa ukoo wa Pashuri: 1247;
42. wa ukoo wa Harimu: 1017.
43. Walawi wa ukoo wa Yeshua, yaani Kadmieli, wazawa wa Hodavia waliorudi kutoka uhamishoni walikuwa 74.
44. Waimbaji: Wazawa wa Asafu walikuwa 148.
45. Walinzi: Wazawa wa Shalumu, wa Ateri, wa Talmoni, wa Akubu, wa Hatita na wa Shobai, walikuwa 138.
46. Koo za wahudumu hekaluni waliorudi kutoka uhamishoni zilikuwa: Ukoo wa Ziha, wa Hasufa, wa Tabaothi;
47. wa Kerosi, wa Siaha, wa Padoni;
48. wa Lebana, wa Hagaba, wa Shalmai;