Agano la Kale

Agano Jipya

Nehemia 11:4-19 Biblia Habari Njema (BHN)

4. Baadhi ya watu wa kabila la Yuda na wa kabila la Benyamini walikaa katika mji wa Yerusalemu. Wafuatao ndio watu wa ukoo wa Yuda waliokaa mjini Yerusalemu: Athaya, mwana wa Uzia, mwana wa Zekaria, mwana wa Amaria, mwana wa Shefatia, mwana wa Mahalaleli. Wote hao ni wazawa wa Peresi.

5. Pia Maaseya, mwana wa Baruku, mwana wa Kolhoze, mwana wa Hazaya, mwana wa Adaya, mwana wa Yoyaribu, mwana wa Zekaria, Mshilo.

6. Wazawa wote wa Peresi waliokaa mjini Yerusalemu walikuwa wanaume mashujaa 468.

7. Watu wa ukoo wa Benyamini waliokaa mjini Yerusalemu ni: Salu, mwana wa Meshulamu, mwana wa Yoedi, mwana wa Pedaya, mwana wa Kolaya, mwana wa Maaseya, mwana wa Ithieli na mwana wa Yeshaya.

8. Baada ya huyo walikuwako Gabai na Salai. Jumla yao 928.

9. Yoeli, mwana wa Zikri, alikuwa ndiye mkuu wao; naye Yuda mwana wa Hasenua alikuwa mkuu wa pili wa mji.

10. Makuhani waliokaa mjini Yerusalemu walikuwa: Yedaya, mwana wa Yoaribu, Yakini,

11. Seraya, mwana wa Hilkia, mwana wa Meshulamu, mwana wa Sadoki, mwana wa Merayothi, mwana wa Ahitubu aliyekuwa msimamizi wa nyumba ya Mungu;

12. hao pamoja na ndugu zao waliofanya kazi hekaluni; walikuwa watu 822. Pamoja na hao, kulikuwa na Adaya, mwana wa Yerohamu, mwana wa Pelalia, mwana wa Amsi, mwana wa Zekaria, mwana wa Pashuri, mwana wa Malkiya;

13. pia kulikuwa ndugu zake waliokuwa wakuu wa jamaa za baba zao; wote pamoja walikuwa watu 242. Pia walikuwako Amaasai, mwana wa Azareli, mwana wa Ahzai, mwana wa Meshilemothi, mwana wa Imeri,

14. pamoja na ndugu zao; wote wakiwa 128, watu mashujaa. Na mkuu wao alikuwa Zabdieli mwana wa Hagedolimu.

15. Nao Walawi waliokaa mjini Yerusalemu walikuwa: Shemaya, mwana wa Hashubu, mwana wa Azrikamu, mwana wa Hashabia, na mwana wa Buni.

16. Shabethai na Yozabadi, wakuu wa ukoo wa Walawi, walikuwa wasimamizi wa kazi za nje ya nyumba ya Mungu,

17. na Matania, mwana wa Mika, mwana wa Zabdi, mzawa wa Asafu, aliyekuwa kiongozi wakati wa kuomba sala za shukrani. Bakbukia alikuwa msaidizi wake. Pamoja nao alikuwako Abda, mwana wa Shamua, mwana wa Galali na mzawa wa Yeduthuni.

18. Walawi wote waliokaa mjini Yerusalemu, mji mtakatifu, walikuwa 284.

19. Wangoja malango waliokaa mjini Yerusalemu walikuwa: Akubu na Talmoni pamoja na ndugu zao waliokuwa wakilinda malango, walikuwa 172.

Kusoma sura kamili Nehemia 11