Agano la Kale

Agano Jipya

Nehemia 11:16-31 Biblia Habari Njema (BHN)

16. Shabethai na Yozabadi, wakuu wa ukoo wa Walawi, walikuwa wasimamizi wa kazi za nje ya nyumba ya Mungu,

17. na Matania, mwana wa Mika, mwana wa Zabdi, mzawa wa Asafu, aliyekuwa kiongozi wakati wa kuomba sala za shukrani. Bakbukia alikuwa msaidizi wake. Pamoja nao alikuwako Abda, mwana wa Shamua, mwana wa Galali na mzawa wa Yeduthuni.

18. Walawi wote waliokaa mjini Yerusalemu, mji mtakatifu, walikuwa 284.

19. Wangoja malango waliokaa mjini Yerusalemu walikuwa: Akubu na Talmoni pamoja na ndugu zao waliokuwa wakilinda malango, walikuwa 172.

20. Watu wengine wa Israeli, makuhani na Walawi walikaa katika miji ya Yuda, kila mmoja katika urithi wake.

21. Lakini watumishi wa hekalu walikaa mjini Yerusalemu katika eneo la Ofeli wakiwa chini ya usimamizi wa Ziha na Gishpa.

22. Kiongozi wa Walawi waliokaa mjini Yerusalemu alikuwa, Uzi, mwana wa Bani, mwana wa Hashabia, mwana wa Matania, mwana wa Mika wa ukoo wa Asafu, waliokuwa waimbaji, viongozi waangalizi wa shughuli za nyumba ya Mungu.

23. Mfalme alikuwa ametoa amri kuhusu zamu zao na mahitaji yao ya kila siku.

24. Pethahia, mwana wa Meshezabeli, wa ukoo wa Zera katika kabila la Yuda, alikuwa mwakilishi kwa mfalme kuhusu mambo yote ya watu wa Yuda.

25. Watu wengine walikaa katika miji karibu na mashamba yao. Baadhi ya watu wa kabila la Yuda walikaa Kiriath-arba, Diboni na Yekabzeeli pamoja na vijiji vilivyoizunguka.

26. Wengine pia walikaa katika miji ya Yeshua, Molada, Beth-peleti,

27. Hasar-shuali na Beer-sheba pamoja na vijiji vilivyoizunguka.

28. Wengine walikaa katika mji wa Ziklagi, Mekona na vijiji vilivyoizunguka.

29. Wengine walikaa katika miji ya Enrimoni, Sora, Yarmuthi,

30. Zanoa na Adulamu pamoja na vijiji vilivyoizunguka, Lakishi na mashamba yaliyouzunguka, na katika Azeka pamoja na vijiji vilivyouzunguka. Hii ina maana kwamba watu wa Yuda walikaa katika eneo lililoko kati ya Beer-sheba upande wa kusini na Bonde la Hinomu upande wa kaskazini.

31. Watu wa kabila la Benyamini walikaa Geba, Mikmashi, Ai, Betheli na vijiji vinavyoizunguka.

Kusoma sura kamili Nehemia 11