Agano la Kale

Agano Jipya

Nehemia 11:10-23 Biblia Habari Njema (BHN)

10. Makuhani waliokaa mjini Yerusalemu walikuwa: Yedaya, mwana wa Yoaribu, Yakini,

11. Seraya, mwana wa Hilkia, mwana wa Meshulamu, mwana wa Sadoki, mwana wa Merayothi, mwana wa Ahitubu aliyekuwa msimamizi wa nyumba ya Mungu;

12. hao pamoja na ndugu zao waliofanya kazi hekaluni; walikuwa watu 822. Pamoja na hao, kulikuwa na Adaya, mwana wa Yerohamu, mwana wa Pelalia, mwana wa Amsi, mwana wa Zekaria, mwana wa Pashuri, mwana wa Malkiya;

13. pia kulikuwa ndugu zake waliokuwa wakuu wa jamaa za baba zao; wote pamoja walikuwa watu 242. Pia walikuwako Amaasai, mwana wa Azareli, mwana wa Ahzai, mwana wa Meshilemothi, mwana wa Imeri,

14. pamoja na ndugu zao; wote wakiwa 128, watu mashujaa. Na mkuu wao alikuwa Zabdieli mwana wa Hagedolimu.

15. Nao Walawi waliokaa mjini Yerusalemu walikuwa: Shemaya, mwana wa Hashubu, mwana wa Azrikamu, mwana wa Hashabia, na mwana wa Buni.

16. Shabethai na Yozabadi, wakuu wa ukoo wa Walawi, walikuwa wasimamizi wa kazi za nje ya nyumba ya Mungu,

17. na Matania, mwana wa Mika, mwana wa Zabdi, mzawa wa Asafu, aliyekuwa kiongozi wakati wa kuomba sala za shukrani. Bakbukia alikuwa msaidizi wake. Pamoja nao alikuwako Abda, mwana wa Shamua, mwana wa Galali na mzawa wa Yeduthuni.

18. Walawi wote waliokaa mjini Yerusalemu, mji mtakatifu, walikuwa 284.

19. Wangoja malango waliokaa mjini Yerusalemu walikuwa: Akubu na Talmoni pamoja na ndugu zao waliokuwa wakilinda malango, walikuwa 172.

20. Watu wengine wa Israeli, makuhani na Walawi walikaa katika miji ya Yuda, kila mmoja katika urithi wake.

21. Lakini watumishi wa hekalu walikaa mjini Yerusalemu katika eneo la Ofeli wakiwa chini ya usimamizi wa Ziha na Gishpa.

22. Kiongozi wa Walawi waliokaa mjini Yerusalemu alikuwa, Uzi, mwana wa Bani, mwana wa Hashabia, mwana wa Matania, mwana wa Mika wa ukoo wa Asafu, waliokuwa waimbaji, viongozi waangalizi wa shughuli za nyumba ya Mungu.

23. Mfalme alikuwa ametoa amri kuhusu zamu zao na mahitaji yao ya kila siku.

Kusoma sura kamili Nehemia 11