Agano la Kale

Agano Jipya

Nahumu 3:3-6 Biblia Habari Njema (BHN)

3. Wapandafarasi wanashambulia,panga na mikuki inametameta;waliouawa hawana idadi,maiti wengi sana;watu wanajikwaa juu ya maiti!

4. Ninewi! Wewe umekuwa kama malaya.Umewashawishi watu, ewe binti wa uchawi,uliyeyafanya mataifa kuwa watumwa kwa umalaya wako,na watu wa mataifa kwa uchawi wako.

5. Mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi nasema nitapambana nawe;nitalipandisha vazi lako hadi kichwani,niyaache mataifa yauone uchi wako,tawala ziikodolee macho aibu yako.

6. Nitakutupia uchafu,na kukutendea kwa dharau,na kukufanya uwe kioja kwa watu.

Kusoma sura kamili Nahumu 3