Agano la Kale

Agano Jipya

Nahumu 3:14-19 Biblia Habari Njema (BHN)

14. Tekeni maji muwe tayari kuzingirwa;imarisheni ngome zenu.Pondeni udongo kwa kuukanyagakanyaga,tayarisheni tanuri ya kuchomea matofali!

15. Lakini huko pia moto utawateketezeni,upanga utawakatilia mbali;utawamaliza kama nzige walavyo.Ongezekeni kama nzige,naam, ongezekeni kama panzi!

16. Wafanyabiashara wako waliongezeka kuliko nyota;lakini sasa wametoweka kama panzi warukavyo.

17. Wakuu wako ni kama panzi,maofisa wako kama kundi la nzige;wakati wa baridi wanakaa kwenye kuta,lakini jua lichomozapo, huruka,wala hakuna ajuaye walikokwenda.

18. Ewe mfalme wa Ashuru, wachungaji wako wamelala,waheshimiwa wako wamesinzia.Watu wako wametawanyika milimani,wala hakuna yeyote wa kuwakusanya.

19. Hakuna wa kuyapa nafuu majeraha yako,vidonda vyako ni vya kifo.Wote wanaosikia habari zako wanashangilia.Maana ni nani aliyeuepa ukatili wako usio na kikomo?

Kusoma sura kamili Nahumu 3