Agano la Kale

Agano Jipya

Mwanzo 3:16-24 Biblia Habari Njema (BHN)

16. Kisha akamwambia mwanamke,“Nitakuzidishia uchungu wa kuzaa,kwa uchungu utazaa watoto.Hata hivyo utakuwa na hamu na mumeo,naye atakutawala.”

17. Kisha akamwambia huyo mwanamume,“Kwa kuwa wewe umemsikiliza mkeo,ukala matunda ya mti ambayo nilikuamuru usile;kwa hiyo, kwa kosa lako ardhi imelaaniwa.Kwa jasho utajipatia humo riziki yako,siku zote za maisha yako.

18. Ardhi itakuzalia michongoma na magugu,nawe itakubidi kula majani ya shambani.

19. Kwa jasho lako utajipatia chakulampaka utakaporudi udongoni ulimotwaliwa;maana wewe ni mavumbi, na mavumbini utarudi.”

20. Adamu akampa mkewe jina “Hawa”, kwani alikuwa mama wa binadamu wote.

21. Mwenyezi-Mungu akawatengenezea Adamu na mkewe mavazi ya ngozi, akawavika.

22. Kisha Mwenyezi-Mungu akasema, “Sasa, binadamu amekuwa kama mmoja wetu, anajua mema na mabaya. Lazima kumzuia kula lile tunda la mti wa uhai, kwani akilila ataishi milele!”

23. Basi, Mwenyezi-Mungu akamfukuza Adamu nje ya bustani ya Edeni, ili akailime ardhi ambamo alitwaliwa.

24. Alimfukuza nje, na kuweka mlinzi upande wa mashariki wa bustani ya Edeni na upanga wa moto uliogeuka huko na huko, kuilinda njia iendayo kwenye mti wa uhai.

Kusoma sura kamili Mwanzo 3