Sura

  1. 1
  2. 2
  3. 3
  4. 4
  5. 5
  6. 6
  7. 7
  8. 8
  9. 9
  10. 10
  11. 11
  12. 12
  13. 13
  14. 14
  15. 15
  16. 16
  17. 17
  18. 18
  19. 19
  20. 20
  21. 21
  22. 22
  23. 23
  24. 24
  25. 25
  26. 26
  27. 27
  28. 28
  29. 29
  30. 30
  31. 31
  32. 32
  33. 33
  34. 34
  35. 35
  36. 36
  37. 37
  38. 38
  39. 39
  40. 40
  41. 41
  42. 42
  43. 43
  44. 44
  45. 45
  46. 46
  47. 47
  48. 48
  49. 49
  50. 50

Agano la Kale

Agano Jipya

Mwanzo 10 Biblia Habari Njema (BHN)

Wazawa wa Noa

1. Baada ya gharika, watoto wa Noa, Shemu, Hamu na Yafethi, walipata watoto wa kiume na wa kike. Hii ndiyo orodha ya wazawa wao:

2. Watoto wa kiume wa Yafethi walikuwa Gomeri, Magogu, Madai, Yavani, Tubali, Mesheki na Tirasi.

3. Watoto wa kiume wa Gomeri walikuwa Ashkenazi, Rifathi na Togama.

4. Watoto wa kiume wa Yavani walikuwa Elisha, Tarshishi, Kitimu na Dodanimu.

5. Hawa ndio asili ya watu walioenea sehemu za pwani, kila watu kwa lugha yao, kwa jamaa zao na kufuata mataifa yao.

6. Watoto wa kiume wa Hamu walikuwa Kushi, Misri, Puti na Kanaani.

7. Watoto wa kiume wa Kushi walikuwa Seba, Hawila, Sabta, Raama na Sabteka. Watoto wa kiume wa Raama walikuwa Sheba na Dedani.

8. Kushi alikuwa baba yake Nimrodi ambaye alikuwa shujaa wa kwanza duniani.

9. Alikuwa mwindaji shujaa mbele ya Mwenyezi-Mungu, ndiyo maana kuna msemo usemao, “Kama Nimrodi mwindaji shujaa mbele ya Mwenyezi-Mungu.”

10. Miji ya kwanza ya utawala wake ilikuwa Babuloni, Ereki na Akadi, katika nchi ya Shinari.

11. Kutoka huko, Nimrodi alikwenda Ashuru, akajenga miji ya Ninewi, Rehoboth-iri, Kala na

12. Reseni ulioko kati ya Ninewi na mji mkubwa wa Kala.

13. Misri alikuwa babu wa Waludi, Waanamu, Walehabi, Wanaftuhi,

14. Wapathrusi, Wakasluhi (ambao ndio asili ya Wafilisti), na Wakaftori.

15. Kanaani alikuwa babu yake Sidoni, mzaliwa wake wa kwanza, na Hethi,

16. na pia babu yao Wayebusi, Waamori, Wagirgashi,

17. Wahivi, Waarki, Wasini,

18. Waarvadi, Wasemari na Wahamathi. Baadaye watu wa jamii mbalimbali za Kanaani walitawanyika,

19. hata eneo la nchi yao likawa toka Sidoni kuelekea kusini, hadi Gerari mpaka Gaza, na kuelekea mashariki hadi Sodoma na Gomora, Adma na Seboimu hadi Lasha.

20. Hao ndio wazawa wa Hamu kadiri ya makabila yao, lugha zao, nchi zao na mataifa yao.

21. Shemu, mkubwa wa Yafethi, alikuwa baba yao Waebrania wote.

22. Watoto wa kiume wa Shemu walikuwa Elamu, Ashuru, Arfaksadi, Ludi na Aramu.

23. Watoto wa kiume wa Aramu walikuwa Usi, Huli, Getheri na Mashi.

24. Arfaksadi alimzaa Shela, Shela akamzaa Eberi.

25. Eberi alikuwa na watoto wa kiume wawili; wa kwanza akamwita Pelegi kwa sababu wakati huo watu duniani waligawanyika, na wa pili akamwita Yoktani.

26. Yoktani alikuwa baba wa Almodadi, Shelefu, Hasarmawethi, Yera,

27. Hadoramu, Uzali, Dikla,

28. Obali, Abimaeli, Sheba,

29. Ofiri, Hawila na Yobabu. Hao wote walikuwa watoto wa Yoktani.

30. Nchi walimokaa ilienea toka Mesha mpaka Sefari katika nyanda za juu za mashariki.

31. Hao ndio wazawa wa Shemu, kadiri ya makabila yao, lugha zao, nchi zao na mataifa yao.

32. Hao ndio jamaa za watoto wa Noa, kadiri ya vizazi vyao na mataifa yao. Kutokana nao mataifa yote yalienea duniani baada ya gharika.