Agano la Kale

Agano Jipya

Mika 7:1-3 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Ole wangu!Hali ilivyo ni kama baada ya mavuno;hakuna tini za mwanzoni ninazotamani.Ni kama wakati wa kuchuma zabibuhakuna hata shada moja la zabibu la kula!

2. Hakuna mcha Mungu aliyebaki nchini,hakuna mtu yeyote mnyofu miongoni mwa watu.Kila mmoja anavizia kumwaga damu;kila mmoja anamwinda mwenzake amnase.

3. Wote ni mabingwa wa kutenda maovu;viongozi na mahakimu hutaka rushwa.Wakubwa huonesha wazi nia zao mbaya,na kufanya hila kuzitekeleza.

Kusoma sura kamili Mika 7