Agano la Kale

Agano Jipya

Mika 1:9-14 Biblia Habari Njema (BHN)

9. Majeraha ya Samaria hayaponyeki,nayo yameipata pia Yuda;yamefikia lango la Yerusalemu,mahali wanapokaa watu wangu.

10. Msiitangaze habari hii huko Gathi,wala msilie machozi!Huko Beth-leafra mgaegae mavumbini kwa huzuni.

11. Nendeni enyi wakazi wa Shafiri,mkiwa uchi na wenye haya.Wakazi wa Zaanani msitoke nje ya mji wenu.Watu wa Beth-ezeli wanalia;msaada wao kwenu umeondolewa.

12. Wakazi wa Marothi wanangojea msaada kwa hamu kubwa,lakini maangamizi yaja kutoka kwa Mwenyezi-Mungukaribu kabisa na lango la Yerusalemu.

13. Enyi wakazi wa Lakishi,fungeni farasi wepesi na magari ya vita.Nyinyi mlikuwa mmeiga dhambi ya watu wa Siyoni,makosa ya Waisraeli yalikuwa kwenu.

14. Hivyo, mnapaswa kuagana na kuwaacha wakazi wa Morasheth-gathi.Nao mji wa Akzibu hautawasaidia wafalme wa Israeli,

Kusoma sura kamili Mika 1