Agano la Kale

Agano Jipya

Mhubiri 9:11-18 Biblia Habari Njema (BHN)

11. Tena, nimeona kitu kimoja hapa duniani, kwamba wenye mbio hawafaulu katika riadha, wala wenye nguvu hawashindi vita; wenye busara hawapati chakula, wenye akili hawatajiriki, wala wenye ujuzi hawapandi vyeo; lakini wakati wa bahati huwapata wote pamoja.

12. Mtu hajui saa yake itafika lini. Kama vile samaki wanavyonaswa katika wavu kwa bahati mbaya, na kama vile ndege wanavyonaswa katika mtego kwa ghafla, ndivyo wanadamu wanavyonaswa na balaa inapowaangukia bila ya kutazamia.

13. Pia hapa duniani nimeona mfano wa hekima, na ulionekana kwangu kuwa wenye maana sana.

14. Palikuwa na mji mmoja mdogo wenye wakazi wachache. Mfalme mmoja mwenye nguvu akafika, akauzingira na kujiandaa kuushambulia.

15. Katika mji huo, alikuwapo maskini mmoja mwenye hekima, ambaye, kwa hekima yake aliuokoa mji huo. Lakini hakuna mtu aliyemkumbuka huyo maskini baadaye.

16. Basi, mimi nasema, hekima ni bora kuliko nguvu, ingawa hekima ya maskini haithaminiwi, na maneno yake hayasikilizwi.

17. Afadhali kusikiliza maneno matulivu ya mwenye hekima,kuliko kusikiliza kelele za mfalme katika kikao cha wapumbavu.

18. Kuwa na hekima ni bora kuliko kutegemea silaha,lakini mwenye dhambi mmoja huharibu mazuri mengi.

Kusoma sura kamili Mhubiri 9