Agano la Kale

Agano Jipya

Mhubiri 7:9-19 Biblia Habari Njema (BHN)

9. Usiwe mwepesi wa hasira,maana, hasira hukaa ndani ya wapumbavu.

10. Usiulize, “Kwa nini nyakati za kale zilikuwa bora kuliko za sasa?”Huulizi hivyo kwa kutumia hekima.

11. Hekima ni ya thamani kubwa kama urithi;ni muhimu kwa wale wote walio hai.

12. Kulindwa na hekima ni kama kulindwa na fedha.Faida ya maarifa ni kwamba hekima hulinda maisha ya mtu aliye nayo.

13. Tafakarini vema kazi yake Mungu;ni nani awezaye kunyosha alichopinda Mungu?

14. Katika siku za fanaka uwe na furaha; katika siku za maafa utafakari jambo hili: Fanaka, pia maafa, Mungu amefanya hiyo ya kwanza iambatane na ya pili ili binadamu asiweze kujua yatakayotukia baada yake.

15. Katika maisha yangu duni, nimeona kila kitu; mtu mwadilifu hufa ingawa ni mwadilifu, ambapo mtu mwovu huendelea kuishi maisha marefu ingawa ni mwovu.

16. Basi, usiwe mwadilifu sana, wala usiwe mwenye hekima mno! Ya nini kujiangamiza wewe mwenyewe?

17. Lakini pia, usiwe mwovu sana wala usiwe mpumbavu! Ya nini kufa kabla ya wakati wako?

18. Inakupasa ushike la kwanza na la pili pia; maana anayemtii Mungu atajengwa kwayo.

19. Hekima humfanya mwenye busara kuwa na nguvu zaidi kuliko watawala kumi mjini.

Kusoma sura kamili Mhubiri 7