Agano la Kale

Agano Jipya

Mhubiri 7:16-25 Biblia Habari Njema (BHN)

16. Basi, usiwe mwadilifu sana, wala usiwe mwenye hekima mno! Ya nini kujiangamiza wewe mwenyewe?

17. Lakini pia, usiwe mwovu sana wala usiwe mpumbavu! Ya nini kufa kabla ya wakati wako?

18. Inakupasa ushike la kwanza na la pili pia; maana anayemtii Mungu atajengwa kwayo.

19. Hekima humfanya mwenye busara kuwa na nguvu zaidi kuliko watawala kumi mjini.

20. Hakika, hakuna mtu mwadilifu duniani atendaye mema daima bila kutenda dhambi.

21. Usitie maanani maneno yote wasemayo wanadamu, usije ukamsikia mtumishi wako akikutukana.

22. Wewe mwenyewe wajua moyoni kwamba umeapiza wengine mara nyingi.

23. Nimeyapima hayo yote kwa hekima; nikajisemea: “Nataka kuwa mwenye hekima!” Lakini hekima iko mbali sana nami.

24. Jinsi gani binadamu ataweza kugundua maana ya maisha; jambo hilo ni zito na gumu mno kwetu!

25. Hata hivyo, nilipania kujua na kuchunguza na kutafuta hekima na maana ya mambo yaliyoko, na pia kujua uovu ni upuuzi, na upumbavu ni wazimu.

Kusoma sura kamili Mhubiri 7