Agano la Kale

Agano Jipya

Mhubiri 7:1-11 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Sifa njema ni bora kuliko marashi ya thamani.Siku ya kufa ni bora kuliko siku ya kuzaliwa.

2. Afadhali kwenda kwenye matanga,kuliko kwenda kwenye karamu,kwa sababu walio hai yawapasa kukumbuka kwamba kifo chatungojea sisi sote.

3. Huzuni ni afadhali kuliko kichekomaana, huzuni ya uso ni faida ya moyo.

4. Moyo wa mwenye hekima huthamini matanga,lakini moyo wa mpumbavu hupenda raha.

5. Afadhali kusikia maonyo ya wenye hekimakuliko kusikiliza nyimbo za wapumbavu.

6. Maana, kicheko cha mpumbavuni kama mlio wa miiba motoni.Hayo nayo ni bure kabisa.

7. Mwenye hekima akimdhulumu mtu;hujifanya mwenyewe kuwa mpumbavukupokea rushwa hupotosha akili.

8. Mwisho wa jambo ni afadhali kuliko mwanzo wake;mvumilivu rohoni ni bora kuliko mwenye majivuno.

9. Usiwe mwepesi wa hasira,maana, hasira hukaa ndani ya wapumbavu.

10. Usiulize, “Kwa nini nyakati za kale zilikuwa bora kuliko za sasa?”Huulizi hivyo kwa kutumia hekima.

11. Hekima ni ya thamani kubwa kama urithi;ni muhimu kwa wale wote walio hai.

Kusoma sura kamili Mhubiri 7