Agano la Kale

Agano Jipya

Mhubiri 5:1-7 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Uwe mwangalifu uendapo katika nyumba ya Mungu, na kukaribia ili kusikiliza kwa makini kuliko kutambika kama watambikavyo wapumbavu, watu wasiopambanua kati ya jema na ovu.

2. Fikiri kabla ya kusema, wala usiwe mwepesi kusema chochote mbele ya Mungu, kwa maana Mungu yuko mbinguni na wewe uko duniani. Kwa hiyo usiseme mengi.

3. Kadiri mtu anavyohangaika zaidi, ndivyo atakavyoota ndoto;sauti ya mpumbavu ni maneno mengi.

4. Ukimwekea Mungu nadhiri, usikawie kuitimiza; na Mungu hapendezwi na wapumbavu. Tekeleza ulichoahidi.

5. Ni afadhali kutoweka nadhiri kuliko kuweka nadhiri kisha usiitimize.

6. Angalia mdomo wako usikuingize dhambini, halafu ikupase kumwambia mjumbe wa Mungu kwamba hukunuia kutenda dhambi. Ya nini kumfanya Mungu akukasirikie na kuiharibu kazi yako?

7. Ndoto zikizidi, kuna maangamizi na maneno huwa mengi. Jambo la maana ni kumcha Mungu.

Kusoma sura kamili Mhubiri 5