Agano la Kale

Agano Jipya

Mhubiri 4:5-13 Biblia Habari Njema (BHN)

5. Mpumbavu hafanyi kazina mwisho hujiua kwa njaa.

6. Ni afadhali kuwa na kidogo tu, pamoja na amani moyoni,kuliko kuwa na mengi, pamoja na taabu;sawa tu na kufukuza upepo.

7. Tena, niliona jambo moja bure kabisa duniani.

8. Nilimwona mtu mmoja asiye na mwana wala ndugu; hata hivyo, haachi kufanya kazi; hatosheki kamwe na mali yake; wala hatulii na kujiuliza: “Ninamfanyia nani kazi na kujinyima starehe?” Hilo nalo ni bure kabisa; ni shughuli inayosikitisha.

9. Ni afadhali kuwa wawili kuliko mtu kuwa peke yake. Kwa sababu wawili watapata tuzo la kazi yao.

10. Ikijatokea mmoja akaanguka, huyo mwenzake atamwinua. Lakini ole wake aliye peke yake akianguka! Huyo hatakuwa na mtu wa kumwinua!

11. Hali kadhalika, wawili wakilala pamoja watapata joto; lakini mtu akiwa peke yake atajipatiaje joto?

12. Mtu akiwa peke yake aweza kushindwa na adui, lakini wakiwa wawili watamkabili na kumshinda adui. Kamba tatu zikisokotwa pamoja hazikatiki kwa urahisi.

13. Afadhali kijana maskini mwenye hekima kuliko mfalme mzee mpumbavu, ambaye hasikilizi shauri jema;

Kusoma sura kamili Mhubiri 4