Agano la Kale

Agano Jipya

Mhubiri 12:1-4 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Umkumbuke Muumba wako siku za ujana wako,kabla hazijaja siku na miaka ambapo utasema:“Sifurahii tena vitu hivyo!”

2. Umkumbuke kabla ya wakati ambapo kwako mwanga wa jua utafifia;mwezi na nyota haviangazi tena,nayo mawingu yametanda tena baada ya mvua.

3. Wakati ambapo mikono inayokulinda inatetemeka,miguu yako imara imepindika,meno yako ya kusagia hayafai kwa uchache,na macho ya kuchungulia dirishani yamefifia.

4. Wakati ambapo milango ya masikio yako imezibika,na sauti za visagio ni hafifu;lakini usiku hata kwa sauti ya ndege utagutuka.

Kusoma sura kamili Mhubiri 12