Agano la Kale

Agano Jipya

Methali 4:9-21 Biblia Habari Njema (BHN)

9. Atakuvika kilemba kizuri kichwani pako,atakupa taji maridadi.”

10. Mwanangu, sikia na kuyapokea maneno yangu,ili upate kuwa na miaka mingi ya kuishi.

11. Nimekufundisha njia ya hekima,nimekuongoza katika njia nyofu.

12. Ukitembea hatua zako hazitazuiwa,wala ukikimbia hutajikwaa.

13. Zingatia mafundisho ya Hekima na usimwache aponyoke,mshike kwa makini maana yeye ni uhai wako.

14. Usijiingize katika njia ya waovu,wala usifuate mwenendo wa watu wabaya.

15. Iepe njia hiyo wala usiikaribie;jiepushe nayo, uende zako.

16. Waovu kamwe hawalali wasipotenda uovu;hawapati usingizi wasipomkwaza mtu.

17. Maana uovu ndicho chakula chao,ukatili ndiyo divai yao.

18. Njia ya watu wema ni kama nuru ya alfajiri,ambayo hungaa zaidi na zaidi hata mchana kamili.

19. Lakini njia ya waovu ni kama giza nene,hawajui kinachowafanya wajikwae.

20. Mwanangu, sikiliza kwa makini maneno yangu,itegee sikio misemo yangu.

21. Usiyaache yatoweke machoni pako,yahifadhi ndani ya moyo wako.

Kusoma sura kamili Methali 4