Agano la Kale

Agano Jipya

Methali 4:20-27 Biblia Habari Njema (BHN)

20. Mwanangu, sikiliza kwa makini maneno yangu,itegee sikio misemo yangu.

21. Usiyaache yatoweke machoni pako,yahifadhi ndani ya moyo wako.

22. Maana hayo ni uhai kwa mtu anayeyapata,ni dawa kwa mwili wake wote.

23. Linda moyo wako kwa uangalifu wote,maana humo zatoka chemchemi za uhai.

24. Tenga mbali nawe lugha potovu;wala midomo yako isitamke maneno madanganyifu.

25. Uyaelekeze macho yako mbele kwa ujasiri,mtazamo wako uwe mbele moja kwa moja.

26. Fikiria njia utakayochukua,na hatua zako zote zitakuwa kamili.

27. Usigeukie kulia wala kushoto;epusha mguu wako mbali na uovu.

Kusoma sura kamili Methali 4