Agano la Kale

Agano Jipya

Methali 4:1-9 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Wanangu, sikilizeni mwongozo wa baba yenu,tegeni sikio mpate kuwa na akili.

2. Maana ninawapa maagizo mema,msiyakatae mafundisho yangu.

3. Mimi pia nilikuwa mtoto mwenye baba,nilikuwa mpole, kipenzi cha mama yangu.

4. Baba yangu alinifundisha hiki:“Zingatia kwa moyo maneno yangu,shika amri zangu nawe utaishi.

5. Jipatie hekima, jipatie ufahamu;usisahau wala kupuuza maneno yangu.

6. Usimwache Hekima, naye atakutunza;umpende, naye atakulinda.

7. Jambo la msingi ni kujipatia hekima;toa vyote ulivyonavyo ujipatie akili.

8. Mthamini sana Hekima, naye atakutukuza;ukimshikilia atakupa heshima.

9. Atakuvika kilemba kizuri kichwani pako,atakupa taji maridadi.”

Kusoma sura kamili Methali 4