Agano la Kale

Agano Jipya

Methali 27:1-6 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Usijisifie ya kesho,hujui nini kitatokea leo mpaka kesho.

2. Acha watu wengine wakusifu,kuliko mdomo wako wewe mwenyewe.

3. Jiwe ni zito na mchanga kadhalika,lakini usumbufu wa mpumbavu ni mzito zaidi.

4. Ghadhabu ni katili na hasira huangamiza;lakini ni nani awezaye kuukabili wivu?

5. Afadhali mtu anayekuonya waziwazi,kuliko yule afichaye upendo.

6. Makaripio ya rafiki yaonesha uaminifu,lakini busu la adui ni udanganyifu.

Kusoma sura kamili Methali 27