Agano la Kale

Agano Jipya

Methali 25:19-24 Biblia Habari Njema (BHN)

19. Kumtegemea mtu asiyeaminika wakati wa taabu,ni kama jino bovu au mguu ulioteguka.

20. Kumwimbia mtu mwenye huzuni,ni kama kuvua nguo wakati wa baridi,au kutia siki katika kidonda.

21. Adui yako akiwa na njaa, mpe chakula;akiwa na kiu, mpe maji ya kunywa.

22. Hivyo utafanya apate aibu kali,kama makaa ya moto kichwani pake,naye Mwenyezi-Mungu atakutuza.

23. Upepo wa kusi huleta mvua,hali kadhalika masengenyo huleta chuki.

24. Afadhali kuishi pembeni juu ya paa,kuliko kuishi nyumbani pamoja na mwanamke mgomvi.

Kusoma sura kamili Methali 25