Agano la Kale

Agano Jipya

Methali 25:13-22 Biblia Habari Njema (BHN)

13. Mjumbe mwaminifu humfurahisha yule aliyemtuma,kama maji baridi wakati wa joto la mavuno.

14. Kama vile mawingu na upepo bila mvua,ndivyo alivyo mtu anayejigamba kutoa zawadi asiitoe.

15. Kwa uvumilivu mtawala huweza kushawishika;ulimi laini huvunja mifupa.

16. Upatapo asali kula kiasi cha kukutosha,usije ukaikinai na kuitapika.

17. Usimtembelee jirani yako mara kwa mara,usije ukamchosha naye akakuchukia.

18. Mtu atoaye ushahidi wa uongo dhidi ya mwenziwe,ni hatari kama rungu, upanga au mshale mkali.

19. Kumtegemea mtu asiyeaminika wakati wa taabu,ni kama jino bovu au mguu ulioteguka.

20. Kumwimbia mtu mwenye huzuni,ni kama kuvua nguo wakati wa baridi,au kutia siki katika kidonda.

21. Adui yako akiwa na njaa, mpe chakula;akiwa na kiu, mpe maji ya kunywa.

22. Hivyo utafanya apate aibu kali,kama makaa ya moto kichwani pake,naye Mwenyezi-Mungu atakutuza.

Kusoma sura kamili Methali 25