Agano la Kale

Agano Jipya

Methali 25:1-16 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Hizi nazo ni methali nyingine za mfalme Solomoni walizonakili watu wa Hezekia, mfalme wa Yuda.

2. Mungu hutukuzwa kwa kuficha mambo,lakini mfalme hutukuzwa kwa yale anayoeleza.

3. Kama zilivyo mbali mbingu na kirefu kina cha ardhindivyo zisivyochunguzika akili za mfalme.

4. Toa takataka katika fedha,na mhunzi atakutengenezea chombo kizuri.

5. Waondoe waovu mbele ya mfalme,na utawala wake utaimarika katika haki.

6. Usijipendekeze kwa mfalme,wala usijifanye mtu mkubwa,

7. maana ni heri kuambiwa, “Njoo huku mbele”,kuliko kuporomoshwa mbele ya mkuu.Mambo uliyoyaona kwa macho yako,

8. usiharakishe kuyapeleka mahakamani;maana utafanya nini hapo baadaye,shahidi mwingine akibatilisha hayo usemayo?

9. Suluhisha ugomvi na mwenzako peke yake,na kila mmoja wenu asitoe siri ya mwenzake;

10. watu wasije wakajua kuna siri,ukajiharibia jina lako daima.

11. Neno lisemwalo wakati unaofaa,ni kama nakshi za dhahabu juu ya madini ya fedha.

12. Onyo la mwenye hekima kwa mtu msikivu,ni bora kuliko pete au vito vya dhahabu safi.

13. Mjumbe mwaminifu humfurahisha yule aliyemtuma,kama maji baridi wakati wa joto la mavuno.

14. Kama vile mawingu na upepo bila mvua,ndivyo alivyo mtu anayejigamba kutoa zawadi asiitoe.

15. Kwa uvumilivu mtawala huweza kushawishika;ulimi laini huvunja mifupa.

16. Upatapo asali kula kiasi cha kukutosha,usije ukaikinai na kuitapika.

Kusoma sura kamili Methali 25