Agano la Kale

Agano Jipya

Methali 23:22-34 Biblia Habari Njema (BHN)

22. Msikilize baba yako aliyekuzaa,wala usimdharau mama yako akizeeka.

23. Nunua ukweli, wala usiuuze;nunua hekima, mafunzo na busara.

24. Baba wa mtoto mwadilifu atajaa furaha;anayemzaa mtoto mwenye hekima atamfurahia.

25. Wafurahishe baba na mama yako;mama aliyekuzaa na afurahi.

26. Mwanangu, nisikilize kwa makini,shikilia mwenendo wa maisha yangu.

27. Malaya ni shimo refu la kutega watu;mwanamke mgeni ni kama kisima chembamba.

28. Yeye hunyemelea kama mnyanganyi,husababisha wanaume wengi kukosa uaminifu.

29. Ni nani wapigao yowe?Ni nani wenye huzuni?Ni nani wenye ugomvi?Ni nani walalamikao?Ni nani wenye majeraha bila sababu?Ni nani wenye macho mekundu?

30. Ni wale ambao hawabanduki penye divai,wale wakaao chonjo kuonja divai iliyokolezwa.

31. Usiitamani divai hata kwa wekundu wake,hata kama inametameta katika bilauri,na kushuka taratibu unapoinywa.

32. Mwishowe huuma kama nyoka;huchoma kama nyoka mwenye sumu.

33. Macho yako yataona mauzauza,moyo wako utatoa mambo yaliyopotoka.

34. Utakuwa kama mtu alalaye katikati ya bahari,kama mtu alalaye juu ya mlingoti wa meli.

Kusoma sura kamili Methali 23