Agano la Kale

Agano Jipya

Methali 23:1-11 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Ukiketi kula pamoja na mtawala,usisahau hata kidogo uko pamoja na nani.

2. Zuia sana hamu yako,ikiwa wewe wapenda sana kula.

3. Usitamani vyakula vyake vizuri,maana vyaweza kukudanganya.

4. Ikiwa unayo hekima ya kutosha,usijitaabishe kutafuta utajiri.

5. Kufumba na kufumbua utajiri hutoweka,huwa kama umepata mabawa ghafla,ukaruka na kutowekea angani kama tai.

6. Usile chakula cha mtu bahili,wala usitamani mapochopocho yake,

7. maana moyoni mwake anahesabu unachokula.Atakuambia, “Kula, kunywa!”Lakini moyoni mwake hayuko pamoja nawe.

8. Utatapika vipande ulivyokula;shukrani zako zote zitakuwa za bure.

9. Usiseme maneno yako mbele ya mpumbavu,maana atapuuza hekima ya maneno yako.

10. Usiondoe alama ya mpaka wa zamani,wala usiingilie mashamba ya yatima,

11. maana Mungu, Mkombozi, ni mwenye nguvu,naye ataitetea haki yao dhidi yako.

Kusoma sura kamili Methali 23