Agano la Kale

Agano Jipya

Methali 22:1-14 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Afadhali kuwa na sifa nzuri kuliko mali nyingi;wema ni bora kuliko fedha au dhahabu.

2. Matajiri na maskini wana hali hii moja:Mwenyezi-Mungu ni Muumba wao wote.

3. Mtu mwangalifu huona hatari akajificha,lakini wajinga hujitokeza mbele wakaumia.

4. Ukinyenyekea na kumcha Mwenyezi-Mungu,utapata tuzo: Fanaka, heshima na uhai.

5. Njia ya waovu imejaa miiba na mitego;anayetaka kuhifadhi maisha yake ataiepa.

6. Mfunze mtoto namna ya kuishi vizuri,naye hatasahau njia hiyo hata uzeeni.

7. Tajiri humtawala maskini;mkopaji ni mtumwa wa mkopeshaji.

8. Apandaye dhuluma atavuna janga;uwezo wake wa kutenda mabaya utavunjwa.

9. Mtu mkarimu atabarikiwa,maana chakula chake humgawia maskini.

10. Mfukuze mwenye dharau na fujo itatoweka,ugomvi na matusi vitakoma.

11. Mwenye nia safi na maneno mazuri,atakuwa rafiki wa mfalme.

12. Mwenyezi-Mungu hulinda elimu ya kweli,lakini huyavuruga maneno ya waovu.

13. Mvivu husema, “Siwezi kutoka nje;kuna simba huko, ataniua!”

14. Kinywa cha mwasherati ni shimo refu;anayechukiwa na Mwenyezi-Mungu atatumbukia humo.

Kusoma sura kamili Methali 22