Agano la Kale

Agano Jipya

Methali 11:4-9 Biblia Habari Njema (BHN)

4. Utajiri haufai kitu siku ya ghadhabu,lakini uadilifu huokoa kutoka kifo.

5. Uadilifu wa watu wanyofu huinyosha njia yao,lakini waovu huanguka kwa uovu wao wenyewe.

6. Uadilifu wa wanyofu huwaokoa na hatari,lakini wafitini hunaswa kwa tamaa zao wenyewe.

7. Mwovu akifa tumaini lake nalo hutoweka;tazamio la asiyemcha Mungu huishia patupu.

8. Mtu mnyofu huokolewa katika shida,na mwovu huingia humo badala yake.

9. Asiyemcha Mungu huangamiza wengine kwa mdomo wake,lakini mwadilifu huokolewa kwa maarifa yake.

Kusoma sura kamili Methali 11