Agano la Kale

Agano Jipya

Methali 11:20-28 Biblia Habari Njema (BHN)

20. Wenye nia mbaya ni chukizo kwa Mwenyezi-Mungu,lakini wenye mwenendo mwema ni furaha yake.

21. Hakika mwovu hataepa kuadhibiwa,lakini waadilifu wataokolewa.

22. Mwanamke mzuri asiye na akili,ni kama pete ya dhahabu puani mwa nguruwe.

23. Matazamio ya waadilifu yana matokeo mema;tamaa za waovu huishia katika ghadhabu.

24. Atoaye kwa ukarimu huzidi kutajirika;lakini bahili huzidi kudidimia katika umaskini.

25. Mtu mkarimu atafanikishwa,amnyweshaye mwingine maji naye atanyweshwa.

26. Watu humlaani afichaye nafaka,lakini humtakia baraka mwenye kuiuza.

27. Atafutaye kutenda mema hupata fadhili,lakini atafutaye kutenda maovu atapatwa na maovu.

28. Anayetegemea mali zake ataanguka,lakini mwadilifu atastawi kama jani bichi.

Kusoma sura kamili Methali 11