Agano la Kale

Agano Jipya

Methali 11:17-31 Biblia Habari Njema (BHN)

17. Mtu mkarimu hufaidika yeye mwenyewe,lakini mtu mkatili hujiumiza mwenyewe.

18. Faida anayopata mwovu ni ya uongo,lakini atendaye mema hakika atapata faida ya kweli.

19. Mtu anayepania kuwa mwadilifu ataishi,lakini anayechagua kutenda maovu atakufa.

20. Wenye nia mbaya ni chukizo kwa Mwenyezi-Mungu,lakini wenye mwenendo mwema ni furaha yake.

21. Hakika mwovu hataepa kuadhibiwa,lakini waadilifu wataokolewa.

22. Mwanamke mzuri asiye na akili,ni kama pete ya dhahabu puani mwa nguruwe.

23. Matazamio ya waadilifu yana matokeo mema;tamaa za waovu huishia katika ghadhabu.

24. Atoaye kwa ukarimu huzidi kutajirika;lakini bahili huzidi kudidimia katika umaskini.

25. Mtu mkarimu atafanikishwa,amnyweshaye mwingine maji naye atanyweshwa.

26. Watu humlaani afichaye nafaka,lakini humtakia baraka mwenye kuiuza.

27. Atafutaye kutenda mema hupata fadhili,lakini atafutaye kutenda maovu atapatwa na maovu.

28. Anayetegemea mali zake ataanguka,lakini mwadilifu atastawi kama jani bichi.

29. Anayeivunja nyumba yake ataambua upepo.Mpumbavu atakuwa mtumwa wa wenye hekima.

30. Matendo ya mwadilifu huleta uhai,lakini uhalifu huuondoa uhai.

31. Ikiwa mwadilifu hupata tuzo hapa duniani,hakika mwovu na mwenye dhambi atapatilizwa.

Kusoma sura kamili Methali 11